Maswaliswali

  • sxas
  • asxa
  • asxa

Mfuko wa pembejeo ni nini

Mfuko wa pembejeo ni taasisi ya Serikali inayojihusisha na ukopeshaji wa zana za kilimo, mifugo na uvuvi.

Masharti ya Mkopo wa Mfuko wa Pembejeo ni yapi?

• Muda wa mkopo ni kati ya miaka 2 mpaka 5 kulingana na aina ya mkopo. • Riba ya Mkopo ni kati ya 6% - 8% kulingana na aina ya mkopo. • Dhamana ya mikopo kwa mwombaji binafsi ni mali isiyohamishika yenye hati miliki au leseni ya makazi. • Kwa vyama vya ushirika au vikundi vya kijamii vilivyosajiliwa sharti viwe na akiba ambayo ni sawa na theluthi moja (1/3) ya mkopo wanaoomba na Halmashauri husika iwe tayari kudhamini theluthi 2 (2/3) ya Mkopo huo. • Mtumishi ana uwezo wa kukopeshwa kwa kudhaminiwa na mwajiri wake.

Nani anatakiwa kukopeshwa na Mfuko wa pembejeo?

Wakulima na wafugaji binafsi, Vikundi vya kijamii vilivyosajiliwa na vyama vya ushirika. Mawakala wa Pembejeo za Kilimo na Mifugo wenye uzoefu usiopungua miaka miwili pamoja na Mifuko ya Pembejeo ya Halmashauri za Wilaya.