Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Pembejeo

AGITF Logo
Historia ya AGITF

Mfuko wa Pembejeo ni taasisi ya Serikali inayotoa mikopo ya Pembejeo za Kilimo/Mifugo na Zana za Kilimo. Mikopo inayotolewa na Mfuko wa Pembejeo ninkwa ajili ya kupanua maeneo ya kilimo na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi. Muda wa mikopo ni kati ya miaka miwili (2) hadi mitano(5) kutegemea aina ya mkopo. Riba ya mkopo ni asilimia sita (6%) hadi nane (8%) kutegemea aina ya mkopo.

Dhamana za mikopo ni hatimiliki au leseni ya makazi ya mali isiyohamishika kwa waombaji binafsi kampuni. Kwa Vyama vya Ushirika na Taasisi za Kijamii zisizo na dhamana zenye hati miliki au leseni za makazi za mali zisizohamishika, dhamana ni akiba za wanachama (30%) na Halmashauri husika (70%). Fomu za maombi ya mikopo zinapatikana kwenye tovuti hii, Ofisi za Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji. Mkopo utaanza kurejeshwa baada ya mwezi mmoja hadi sita. Fedha ya Mkopo italipwa kwenye Kampuni ya chaguo la mwombaji.

WALENGWA WA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA PEMBEJEO

Walengwa ni;

1. Wakulima binafsi.

2. Makampuni.

3. Vikundi na Taasis i za Kijamii zilizosajiliwa na zinazojishughulisha na Kilimo.

4. Wasambazaji wa pembejeo za kilimo,mifugo na Uvuvi.

5. Wenye viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya Kilimo,mifugo na uvuvi.