Historia


Mfuko wa Pembejeo ni taasisi ya Serikali inayotoa mikopo ya Pembejeo za Kilimo/Mifugo na Zana za Kilimo. Mikopo inayotolewa na Mfuko wa Pembejeo ninkwa ajili ya kupanua maeneo ya kilimo na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo/mifugo. Muda wa mikopo ni kati ya miaka miwili hadi mitano kutegemeanaina ya mkopo. Riba ya mkopo ni asilimia sita (6%) hadi nane (8%) kutegemea aina ya mkopo na mkopaji.

Dhamana za mikopo ni hatimiliki au leseni ya makazi ya mali isiyohamishika kwa waombaji binafsi kampuni. Kwa Vyama vya Ushirika na Taasisi za Kijamii zisizo na dhamana zenye hati miliki au leseni za makazi za mali zisizohamishika, dhamana ni akiba za wanachama (30%) na Halmashauri husika (70%). Fomu za maombi ya mikopo zinapatikana Ofisi za Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji. Mkopo utaanza kurejeshwa baada ya mwezi mmoja hadi sita. Fedha ya Mkopo italipwa kwenye Kampuni ya chaguo la mwombaji.