Mikopo ya Miundombinu ya kilimo Mifugo na uvuvi


Ni Mkopo wa Miaka Mitatu unaotolewa kwa wakulima binafsi,vikundi,Vyama vya ushirika.

Riba yake ni 6% mpaka 7% kwa Mwaka.

• Mwombaji atajaza Fomu ya maombi inayopatikana katika Ofisi ya Mfuko wa Pembejeo,Ofisi

za Kilimo katika Halmashauri zote nchini pamoja na Tovuti ya Mfuko wa Pembejeo.

• Mwombaji aandae andiko la mradi (Business plan) linalochambua mahitaji yake, mizania

• ya biashara,mapato na faida.

• Mwombaji atatakiwe aambatanishe Ankara ya kifani ”Profoma Invoice” kutoka kwa Mgavi na malipo yatafanywa moja kwa moja kwa mgavi wa bidhaa husika.

• Dhamana ya mkopo kwa mwombaji binafsi au Kampuni ni mali isiyohamishika yenye hati miliki (title deed) au leseni ya makazi inayokubalika Kisheria.

• Dhamana ya mkopo kwa Vyama vya Ushirika naTaasisi za Kijamii zisizo na dhamana zenye hatimiliki au leseni za makazi za mali zisizo hamishikani akiba za wanachama (30%) na Halmashauri ambapo ushirika upo (70%).

• Dhamana ya mshahara, Mwombaji atawasilisha maombi yakiwa yameambatanishwa na kivuli cha mkataba wa ajira (Employment Contract /Introductory letter), hati za malipo ya mishahara yake angalau miezi sita mfululizo, Nakala za kitambulisho rasmi. Marejesho ya mkopo yatafanywa na mwajiri kila mwezi kutoka katika mshahara wa mkopaji na kuwasilisha kwenye akaunti za Mfuko wa Pembejeo moja kwa moja.