Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mfuko wa Pembejeo

AGITF Logo
Aina za Mikopo na Taratibu zake
30 Jun, 2023

1. Pembejeo za Kilimo, Mifugo na Uvuvi - Mwombaji/Kikundi atajaza fomu ya maombi ya Mkopo ambapo fomu iliyokamilishwa itaidhinishwa na Halmashauri husika anakofanyia shughuli inayoombewa mkopo . Muda wa mkopo ni miaka miwili (2) na riba ni 8% kwa mtu binafsi na 6% kwa vikundi.

2. Mitambo ya mashambani (Farm Machinery)

Mkop huu unajumuisha matrekta mapya, zana za kuvunia na kupandia, magari ya kubeba mazao, mashine za kukamulia maziwa, kupakia miwa, kufyeka na kufungia nyasi, kutengeneza chakula cha Mifugo.

Mkopaji atatakiwa kuchangia ununuzi wa mtambo husika kwa asilimia kumi (10%). Muda wa mkopo ni miaka 5 ikijumuisha na muda wa rehema (grace period) na riba ni 7% kwa mtu binafsi na 6% kwa vikundi.

3.Matrekta ya mikono ( Power Tiller) – Muda wa mkopo ni miaka mitatu (3) ikijumuisha na muda wa rehema (grace period). Riba ni 6% kwa Vikundi na 7% kwa mtu binafsi.

4. Ukarabati wa Matrekta

Muda wa Mkopo ni miaka miwili (2) ikijumuisha na muda wa rehema (grace period). Riba ni 6% kwa mtu binafsi 7% kwamtu binafsi na 6% kwa vikundi.

5. Mikopo ya miundo mbinu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi – Hii ni pamoja na maghala, shamba kitalu (green house) nyumba ya shambani, mabanda ya kuku/ng’ombe/nguruwe, mizinga ya nyuki,visima,mabwawa,vifungo vya kutibia na kuogeshea mifugo,mashimo ya kutunza vyakula vya mifugo.

Muda wa mkopo ni miaka mitatu (3) na miezi sita ikijumuisha muda wa rehema na riba ni 7% kwa mtu binafsi na 6% kwa vikundi.

6.Mikopo ya Fedha za kuendeshea shughuli za shamba (Farm Operation)

Muda wa Mkopo ni miaka 2 na miezi 6 ikijumuisha na muda wa rehema. Riba ni 7% kwa watu binafsi na 6% kwa vikundi. Ardhi iwe inamilikiwa kisheria na mkopaji awe na uzoefu wa kutosha katika shughulianayokusudia kuifanya.

7. Zanaunganishi (Farm Implements)

Hizi ni trailers,harrows,dis ploughs boesaw,carcass saw, spitting, ban water pump, storage and cold chain equipments chiller, insulated container,meat van, deepfrezers, retrigerators, liquid nitrogen containers, coolboxers, and cans.

Muda wa mkopo ni miaka 3 ikijumuisha na muda wa rehema wa miezi 6 na riba ni 7% kwa mtu binasi na 6% kwa vikundi.

8.Mikopo ya kununua ardhi kwa ajili ya kilimo, ufugaji na uvuvi.

Muda wa mkopo ni miaka 4 ikijumuisha na muda wa rehema wa miezi 12 na riba ni 7% kwa mtu binafsi na 6% kwa vikundi. Ardhi iwe inamilikiwa kisheria na mkopaji awe na uzoefu wa kutosha katika shughuli anayokusudia kuifanya.

9. Mikopo ya zana za kusindika na Vifungashio vya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Muda wa mkopo ni miaka 3 ikijumuisha na muda wa rehema wa miezi 6 na riba ni7% kwa mtu binafsi na 6% kwa vikundi.

10.Mikopo kwa taasisi kwa kukopesha (on lending/wholesale)

Riba ya mkopo ni asilimia nne (4%) na Taasisi (Asasi husika itamkopesha mkulima kwa riba ya asilimia sita (6%) kwa maka. Muda wa Mkop ni miaka 3 ikijumuisha na muda wa rehema wa miezi sita (6).